Home Habari za michezo BAADA YA KUPEWA ‘THANK YOU’ …MKUDE ATUMIKA KUITISHA SIMBA….YANGA WATAMBA KUTIBUA MAMBO..

BAADA YA KUPEWA ‘THANK YOU’ …MKUDE ATUMIKA KUITISHA SIMBA….YANGA WATAMBA KUTIBUA MAMBO..

Tetesi za Usajili Yanga

Uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa licha ya utani wa jadi uliopo baina yao na Simba SC bado kuna jambo wanalisikitikia hasa kumuacha kiungo mzoefu, Jonas Mkude.

Mkude Juni 22, ‘Thank You’ kutoka Simba SC ilipita naye baada ya mkataba wake kuisha hivyo kwa sasa yupo huru akitajwa kuwa kwenye rada za watani zao wa jadi, Young Africans.

Ikumbukwe kwamba nyota huyo alipandishwa kutoka timu ya vijana ya Simba SC akiwa ni mchezaji aliyedumu kwa muda wa miaka 13 chini ya Kocha Seleman Matòla ambaye kwa sasa anafundisha timu za vijana.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe, ameweka wazi kuwa “Unapomzungumzia Mkude (Jonas) yule ni kiungo mzuri na uzoefu kumuacha kirahisi ujue inahitaji kuwe na sababu maalumu lakini haizuii kusema kuwa ni mchezaji mzuri.

“Watani zetu wa jadi kwa wanachokifanya sasa acha tusubiri ninadhani msimu ujao watakuwa na kumbukumbu nzuri kwa kuwa watapata majuto na ninachojua mimi Mkude kwenye timu yoyote ile anacheza,” amesema Kamwe.

Gwiji mwingine ambaye hayupo na Simba SC ni Erasto Nyoni ambaye huyu ametambulishwa ndani ya kikosi cha Namungo.

SOMA NA HII  BAADA YA NAMUNGO KUFUNGWA JUZI...JULIO KAONA ISIWE TABU AISEE...KAFUNGUKA HAYA...AITAJA YANGA TENA...