Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MABOSI SIMBA KUMPANGIA KOCHA KIKOSI…JEMEDARI SAID AFUNGUKA MAPYA …

KUHUSU ISHU YA MABOSI SIMBA KUMPANGIA KOCHA KIKOSI…JEMEDARI SAID AFUNGUKA MAPYA …

Habari za Simba

Mchambuzi wa Soka, Jemedari Said amesema kuwa viongozi wa baadhi ya vilabu vya soka nchini wamekuwa na tabia ya kutowajali wachezaji wao jambo linalosababisha mvurugano baina ya klabu na mchezaji.

Jemedari amesema hayo kufuatia kauli ya aliyekuwa kiungo wa Simba Sc, Nelson Okwa kudai kuwa amepotezewa muda mwingi na klabu hiyo na kwamba alikuwa hapangwi kucheza mechi bila sababu za msingi.

“Watu walimsikia Feitoto wakampinga na wengine wakadhani ni Yanga tu, leo Okwa anasema Simba viongozi wanakuja na karatasi imeandikwa majina ya wanaoanza kabisa huko huko. Hili kwenye vilabu vyetu hasa Simba na Yanga sio jambo geni, tushasikia mengi zaidi ya haya.

“Watu wanampangia kocha wa timu ya taifa nani aitwe nani asiitwe, nani acheze na nani asicheze, tukiwaambia mnasema hatuwapendi, au hatakama ni kweli kwanini useme sasa. Ukiwakuta akina Okwa ndo wanapasuka kama hivyo.

“Mimi nafikiri hoja hapa ni je kweli Simba viongozi wanampangia kocha list mpaka sasa mwaka 2023? Unajiuliza kitendo cha Ally Salim kucheza mbele ya Beno Kakolanya, je, nacho ni katika hiyo hali ya kupangiana timu?

“Kama hili linafanyika nadhani halina maslahi kwa mpira wetu. Unampangia timu kocha halafu akifungwa unamfukuza au unafukuza viongozi?” amesema Jamedari Said.

SOMA NA HII  KIMENUKA SIMBA...DEWJI ATANGAZA KUMTAMBUA MGUNDA KAMA KOCHA MKUU WA TIMU...