Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUTUA JKT…DILUNGA AFUNGUKA MAPYA KUHUSU ISHU YAKE NA...

SIKU CHACHE BAADA YA KUTUA JKT…DILUNGA AFUNGUKA MAPYA KUHUSU ISHU YAKE NA SIMBA…

Habari za Michezo leo

Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na maafande wa JKT Tanzania kiungo wa pembeni wa zamani wa Simba SC, Hassani Dilunga ‘HD’ amekiri kuwa Simba SC haina baya kwake na anaitakia kila la heri kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24.

Kiungo huyo ambaye alicheza Simba SC kwa misimu mitatu, ameingia kandarasi ya miaka miwili ikiwa ni miezi kadhaa tangu kurudi uwanjani baada ya kuuguza jeraha la goti kwa msimu mmoja.

Dilunga amesema kuwa baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu anahitaji kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza mara kwa mara ili aweze kurejea kwenye ubora wake.

“Niliongea vitu kadhaa na Kocha Roberto Oliviera, nikazungumza na uongozi tukakubaliana, sina vingi sana naweza kuvielezea badala yake ninachojua kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, Simba SC hawana baya kwangu.

“Wamenisaidia sana kipindi cha matibabu hadi napona, wanaonijua Dilunga wanatambua ukweli ni upi, nimekaa chini na familia yangu nikaona acha iwe zamu ya JKT Tanzania,” amesema Dilunga.

Amesema ni kweli kuna raha yake kuichezea Simba, lakini wakati mwingine mengine yanabaki ya ndani anawatakia Simba msimu mzuri kwani anajua aliifanyia kila kitu na ilimthamini hivyo ni wakati wa kutafuta changamoto nyingine.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA NGAO YA JAMII ....MANULA APEWA SIKU SABA KWA YANGA...KOCHA AFUNGUKA ATAKACHOMFANYA..