BIASHARA United hawa Wanajeshi wa Mpakani wametinga hatua ya awali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dikhili FC.
Ni mabao ya Ramadhan Chombo wengi hupenda kumuita Redondo ambaye aliweza kuyazamisha kimiani yote katika Uwanja wa Azam Complex.
Ilikuwa ni mapema dakika ya 19 na 23 aliweza kuzamisha nyavuni huku akikosa bahati ya kupachika penalti dakika dakika ya 27 ambayo ingemfanya aweze kusepa na mpira wake kwa kufunga hat trick.
Penalti hiyo Redondo alipiga kwa umakini ila iligonga mwamba na kufanya akwame kutimiza malengo yake ya kuweza kuipa bao la tatu timu yake ya Biashara United.
Katika mchezo wa kwanza ugenini Biashara United ilishinda kwa bao 1-0 hivyo jumla inasonga mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.