Home news BAADA YA KUVURUNDA MECHI NA NAMUNGO..NABI AIBUKA NA STAILI MPYA YANGA…AUCHO KAMA...

BAADA YA KUVURUNDA MECHI NA NAMUNGO..NABI AIBUKA NA STAILI MPYA YANGA…AUCHO KAMA KAWA…


Ni wazi kwamba mechi iliyopita Yanga haikuonesha soka la kuwavutia mashabiki wakati ikikipiga dhidi ya Namungo, sasa unaambiwa mazoezi ya jana ilikuwa ni gusa achia, huku kiungo wake Khalid Aucho akiteka mashabiki.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa uwanja wa Ilulu, Yanga iliambulia sare ya bao 1-1 huku wakitokea nyuma kabla ya kusawazisha kwa mkwaju wa penalti.

Yanga ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa kwenye Ligi Kuu NBC na kukaa usukani kwa pointi 16, inajiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Mbeya Kwanza utakaopigwa Jumanne katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mabingwa hao wa kihistoria wamewasili jana asubuhi ambapo baada ya kupumzika kwa masaa kadhaa wameendelea na mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jeshi kujiweka fiti.

Katika mazoezi hayo chini ya benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Nassredin Nabi pamoja na kupasha misuli lakini muda mwingi aliutumia kwa wachezaji kupigiana pasi.

Awali Nabi aliwagawa wachezaji makundi matatu kwa ajili kunyoosha miili, kabla ya kuwapa zoezi hilo la kugusa mpira mara moja, huku Aucho aliyekosekana mchezo uliopita akionesha vitu safi.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki waliopenya kuingia uwanjani hapo, hawakusita kuwataja nyota, Aucho, Heritier Makambo na Feisali Salum wakitikisa vichwa wakimaanisha kukubali uwezo wao.

Mazoezi hayo yalidumu kwa takribani masaa mawili huku Injinia Heris Said akiwa sambamba na timu hiyo mwanzo mwisho kufuatilia matizi hayo.

SOMA NA HII  KAMATA PESA YA KUFUNGIA MWAKA NA SLOT YA UHAKIKA KUTOKA MERIDIANBET CASINO.....