Home Uncategorized NAMUNGO WAIPIGIA HESABU NDEFU MBAO FC

NAMUNGO WAIPIGIA HESABU NDEFU MBAO FC


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa kwa sasa unarejea kwenye uwanja wao wa nyumbani, Majaliwa maarufu kuiandalia dozi Mbao FC kwenye mchezo wao wa ligi.

Namungo, Januari 12, 2020 kwenye mchezo wake wa ligi ilipindua meza kibabe mbele ya Tanzania Prisons iliyokuwa inaongoza kwa mabao 2 kipindi cha kwanza ila mwisho Namungo ilishinda kwa mabao 3-2.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery aliema kuwa wanatambua ugumu wa ligi ulivyo watapambana kuendelea kupata matokeo mazuri.
“Tunarudi nyumbani na tutakuwa na mchezo kwanza wa Kombe la FA dhidi ya Biashara United kisha itakuwa ni zamu ya Mbao na Alliance, tunajipanga kufanya vizuri ukizingatia tutakuwa nyumbani mashabiki watupe sapoti,” alisema Thiery.
Februari mosi, Namungo itamenyana na Mbao FC ya Mwanza uwanja wa Majaliwa.

SOMA NA HII  KOSI HILI LA MASTAA KARANTINI INAWAHUSU