Home news PAMOJA NA KUSEPA YANGA…MUKOKO ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA YA MOYONI …AWATAJA VIONGOZI…

PAMOJA NA KUSEPA YANGA…MUKOKO ASHINDWA KUJIZUIA..AANIKA YA MOYONI …AWATAJA VIONGOZI…


Baada ya kuthibitishwa ameondoka Young Africans na kusajiliwa TP Mazembe ya nchini kwao DR Congo, Kiungo Mkabaji Mukoko Tomombe ametoa ya moyoni.

Mukoko ameondoka Young Africans akisisitiza kuipenda klabu hiyo iliyomsajili mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea AS Vita ya ya mjini Kinshasa-DR Congo.

Kiungo huyo amesema daima klabu hiyo Kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itaendelea kubaki moyoni mwake, kufuatia maisha mazuri aliyoishi klabuni hapo.

Amesema aliishi vizuri na wachezaji wenzake, viongozi, mashabiki na wanachama, hivyo alijihisi yupo nyumbani katika kipindi chote alichokaa Young Africans.

Maneno hayo ya mapenzi ya dhati kwa Mukoko dhidi ya Young Africans, ameyaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram , ambapo dili lake la kuondoka Young Africans lilishika hatamu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Yanga ni kama familia kwangu. Siku zote itabaki moyoni. Nitaikumbuka Tanzania hasa kwa ugali na samaki wa baharini.“ Teacher @mukoko_tunombe

SOMA NA HII  MASOUD DJUMA AANZA KWA MKWARA MZITO DODOMA JIJI...AWAKIMBIZA WACHEZAJI MCHAKAMCHAKA JUANI...