Home Habari za michezo JEMEDARI SAID: INAKERA…YANGA WAKISHINDA WAMENUNUA MECHI… ILA SIMBA NI SAWA..?

JEMEDARI SAID: INAKERA…YANGA WAKISHINDA WAMENUNUA MECHI… ILA SIMBA NI SAWA..?

Habari za Simba

Baada ya kuzuka kwa tabia ya watu kuzusha maneno ya rushwa pindi timu za Simba na Yanga zinapopata matokeo mbele ya timu zingine za Ligi Kuu Tanzania Bara.

mchambuzi mahiri wa masuala ya Soka Jemedari said ameibuka na kukemea suala hilo huku akusisitiza ubora wa vikosi hivyo , walimu wenye uwezo ndio hasa siri ya kufanya vyema katika michezo yao.

“imeanza kuudhi Simba wakishinda na Yanga wakishinda. Linatokea kundi la watu unaowaamini na wanasema kuwa ushindi huo una makandokando ya Rushwa. Umefika muda wa wadau kutoa ushirikiano kwa Vyombo vya Uchunguzi. Watu ni kama vile hawaamini tena kama timu zetu zinaweza kushinda kwa kushindana kiwanjani. Wanaoamini kama kuna mambo hayo watoe ushirikiano. Kama hawawezi kutoa ushirikiano hakuna sababu ya haya mambo kuzungumzwa. Mimi nimecheza mpira, mkiwa mmeshinda kisha anatokea mtu na kuanza kuutia dosari ushindi wenu inauma. Hata mchezaji aliyefunga Hatrick hajisikii vizuri. Wadau watoe ushirikiano, kama hawawezi wakae kimya’.

SOMA NA HII  SAKATA LA MORRISON KUACHWA KIMYA KIMYA SIMBA...EDO KUMWEMBE AIBUKA NA HILI...AMTAJA HANS POPE ...