Home Uncategorized NAMUNGO WATUSUA KIMATAIFA,NGOMA UGENINI YAWA 3-3

NAMUNGO WATUSUA KIMATAIFA,NGOMA UGENINI YAWA 3-3

 


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Namungo FC wameendelea kupambana kimataifa kwa kuweza kutinga hatua ya tatu ya kombe hilo baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya El Hilal Obei ya Sudan.


Licha ya sare ya leo kwenye Uwanja wa Al Hilal, Namungo inapenya kwa kuwa ilishinda mchezo wa kwanza mabao 2-0, Uwanja wa Azam Complex.


Namungo ingepoteza leo nafasi ya kushinda mbele ingekuwa haina wa kumlaumu kwa kuwa wachezaji wote kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam walikiri kuwa walikosa nafasi nyingi za wazi ambazo walizipata.


Inashinda kwa jumla ya mabao 5-3 na imekuwa na faida pia ya kupata abao ugenini jambo linaloonyesha kwamba walipambana mwanzo mwisho.

Watupiaji walikuwa kwa Namungo ni Stephen Sey dakika ya 2, Bigirimana Blaise dakika ya 38 na beki wa kushoto Edward Manyama aliweka usawa dakika ya 49.


Ushindi huo unaifanya Namungo kutinga hatua ya tatu ikisubiri wale watakaopoteza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ili wapangiwe timu ambayo watacheza nayo.

Mechi mbili, moja ya nyumbani na ugenini ikiwa watashinda watakata tiketi ya kutinga hatua ya makundi ndani ya Kombe la Shirikisho. 

SOMA NA HII  AZAM FC WASISITIZA KUWA WANA JAMBO LAO