Home Uncategorized VITA YA UFUNGAJI BORA MAMBO NI MOTO, AZAM YAPACHIKA WAWILI,

VITA YA UFUNGAJI BORA MAMBO NI MOTO, AZAM YAPACHIKA WAWILI,

 


KWENYE orodha ya wafungaji Bongo nyota wa timu ya Azam FC, Prince Dube ni kinara wa kutupia akiwa nayo mabao sita na ametoa jumla ya pasi nne za mwisho.


Azam FC kwa sasa ikiwa imefunga mabao 14 yeye amehusika kwenye mabao 10 kwa kuwa amefunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao.

Vita yake kwenye ufungaji ni dhidi ya mshambuliaji bora wa msimu uliopita, Meddie Kagere wa Simba ambaye yeye ana mabao manne kibindoni.

Msimu uliopita Kagere alitupia mabao 22 na kutwaa tuzo ya mfungaji bora.


Pia orodha inaongezeka ndani ya Azam FC uwepo wa jina la Obrey Chirwa mwenye mabao manne ndani ya ligi na ana pasi mbili za mabao.

Pia Chris Mugalu na Bigirimana Blaise wa Namungo FC hawa wote wametupia mabao matatu matatu sawa na Kelvin Friday wa Biashara United.

Nyota mwingine mwenye mabao matatu ambaye ni mzawa anaitwa Yusuph Mhilu yeye anacheza ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.


Meshack Abrahm wa Gwambina FC naye ni miongoni mwa washambuliaji wenye ushkaji na nyavu kwa kuwa ametupia mabao matatu.


Kwa upande wa mabeki kinara wa kutupia ni Lamine Moro wa Yanga yeye ametupia mabao mawili. 

SOMA NA HII  OLIVIER GIROUD YUPO KARIBU KUTIMKIA ITALIA