Home Uncategorized YANGA YATOSHANA NGUVU NA JAMHURI KOMBE LA MAPINDUZI

YANGA YATOSHANA NGUVU NA JAMHURI KOMBE LA MAPINDUZI


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wamekutana na timu nzuri ndani ya Uwanja wa Amaan jambo lililowafanya walazimishe sare ya bila kufungana.

Mchezo wa leo wa Kombe la Mapinduzi ambao ni wa makundi ikiw ipo kundi A pamoja na timu ya Namungo umekamilika kwa dakika 90 kwa timu zote mbili zilizokuwa uwanjani ambazo ni Yanga na Jamhuri kutoshana nguvu bila kufungana.

Shukrani kwa kipa namba moja wa Jamhuri, Nasoro Twaliba ambaye alikuwa na kazi ya kuokoa mashuti ya Wazir Junior ambaye alikosa utulivu kipindi cha kwanza pamoja na Yacouba Songne ambaye naye alishindwa kupachika bao kutokana na uimara wa kipa wa Jamhuri.

Pia kipa wa Yanga , Farouk Shikalo naye alikuwa makini kulinda lango lake ambapo aliokoa michomo ya  Ally Juma pamoja na Yunus Makame ndani ya uwanja.

Kaze amesema:”Tumekutana na timu bora na imara jambo ambalo limefanya tupate matokeo haya, kwa kuwa ni mwanzo bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo,” .

Mchezaji bora wa mchezo wa leo Juma Ally wa Klabu ya Jamhuri ya Zanzibar ambaye amepewa zawadi ya laki mbili amesema kwake ni furaha kuwa mchezaji bora na anaamini watazidi kupambana kwa ajili ya mechi zijazo.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA KMC