Home Uncategorized KOCHA LIVERPOOL ASHAURIWA KUSAJILI BEKI WA KATI

KOCHA LIVERPOOL ASHAURIWA KUSAJILI BEKI WA KATI


 BEKI wa zamani wa Klabu ya Liverpool, Jamie Carragher amesema kuwa itakuwa ngumu kwa timu hiyo kuweza kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa haitasajili beki wa kati kwenye dirisha la usajili wa mwezi Januari.

Beki huyo ambaye alicheza ndani ya kikosi hicho msimu wa 1996-2013 na kucheza jumla ya mechi 508 na kutupia mabao manne kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya michezo ameyasema hayo baada ya timu hiyo kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Southampton.


Kupoteza mchezo huo kunaifanya Liverpool ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 kuwa na pointi 33 sawa na Manchester United ambayo ikishinda mchezo wake dhidi ya Burneley wikendi hii inakuwa na uhakika wa kushika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa kuwa imecheza michezo 16.

Bao pekee la ushindi Uwanja wa St. Mary’s lilifungwa na Danny Ings dakika ya pili jambo lililofanya beki huyo kumshauri Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp kuhakikisha kwamba anatafuta beki ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa kuwa mabeki wake wengi wanasumbuliwa na majeruhi.


SOMA NA HII  MAURIZIO SARRI ATIMKA CHELSEA AIBUKIA JUVENTUS