Home Habari za michezo HUYU NDIYE IBRAHIM BACCA….MKIMYA MWENYE MIGUU INAYOONGEA…

HUYU NDIYE IBRAHIM BACCA….MKIMYA MWENYE MIGUU INAYOONGEA…

Habari za Yanga SC

Yanga hawajakosea kusema watamuongeza Mkataba na Mshahara mlinzi wake Ibrahim Bacca. Kiwango anachokionesha ndio msemaji wake mkuu kwa sasa.

Ni beki aliyekamilika kwa Kila kitu, mipira ya juu anaruka, chini anasimama mguu wa kulia anapiga, mguu wa kushoto anapiga pia, ni adui wa kila mshambuliaji wa timu pinzani mshambuliaji akitaka kwenda kwa nguvu atakutana na uso wa huyu beki hapa yanga walilamba dume.

Kwa Ufupi Yanga walifanya usajili ulio bora zaidi kwa beki huyu wa kati asiye na papara akiwa kwenye majukumu yake.

Mwaka 2017 wakati Zanzibar Heroes inacheza fainali kwenye Mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup pale Machakos nchini Kenya, mwaka ule kilipotangazwa kikosi cha Zanzibar Heroes wengi walishangazwa kumuona kocha Hemed Suleiman (Morocco) kumwita katika kikosi kile Ibrahim Bacca kwa vile walikuwa hawamjui na alikuwa mdogo mno kipindi kile akiwa na umri wa miaka 19.

Kumbe kocha Morocco alikiona mbali kipaji chake. Anaitwa Ibrahim Abdallah Hamad (Ibra Bacca) beki kisiki kisichokuwa na papara.

Tayari ashaipeleka Yanga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, na tayari washatanguliza mguu Fainali ya Shirikisho Afrika na bila shaka Nabi atampa jukumu pia katika mchezo wa marudiano siku ya Jumatano kwani namba zake zinambeba ndani ya kikosi cha Yanga kwa sasa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI LIGI KUU DHIDI YA AZAM....'SURE BOY' KAONA ISIWE TABU..KAAMUA KUFUNGUKA YOTE..