Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI LIGI KUU DHIDI YA AZAM….’SURE BOY’ KAONA ISIWE...

KUELEKEA MECHI LIGI KUU DHIDI YA AZAM….’SURE BOY’ KAONA ISIWE TABU..KAAMUA KUFUNGUKA YOTE..


KIUNGO wa Yanga, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ amewachimba mkwara mabosi wake wa zamani Azam FC kwa kuwaambia kuwa atahakikisha anaipambania timu yake kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kupigwa Aprili 6, mwaka huu.

Sure Boy ni mchezaji wa zamani wa Azam, amejiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili, anatarajia kucheza na timu yake zamani katika mchezo huo unaotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Yanga wanaongoza ligi kwa pointi 48 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 37 wakati Azam wakiwa na pointi 28 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. Akizungumza na Championi Jumatano, Sure Boy alisema: “Ni kawaida kucheza na timu yangu ya zamani kwa sababu hakuna ambacho kitaongezeka zaidi ya kutakiwa kupambania timu kufikia malengo ya ubingwa kwa kuweza kupata ushindi katika huo mchezo ambao tunaamini hautokuwa mwepesi kwa timu zote.

“Nawaheshimu kwa sababu walikuwa mabosi wangu zamani ila kwa sasa ni mchezaji wa klabu nyingine ambayo natakiwa kuhakikisha natimiza malengo ya timu kwa kuhakikisha timu inapata matokeo katika hali yoyote ili kuweza kufikia malengo ya ubingwa katika msimu huu.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA WAGHANA JANA....GAMONDI ASHTUKIA JAMBO HILI KWA MASTAA WAKE..