Home Habar za Usajili Simba KULEKEA MECHI YA JUMAPILI DHIDI YA USGN..PABLO AIBUKA NA HILI TENA…AJIPA JUKUMU...

KULEKEA MECHI YA JUMAPILI DHIDI YA USGN..PABLO AIBUKA NA HILI TENA…AJIPA JUKUMU KWA MASHABIKI…


Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Pablo Franco ameweka wazi kuwa wanahitaji kupata ushindi katika mchezo wao wa jumapili wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie ili kuwapa furaha mashabiki wao.

Kauli hiyo imesemwa na Pablo kuwa anaamini mashabiki watajitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa hiyo itakuwa jambo zuri kushinda ili kusherehekea kwa pamoja.

“Tunajua tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu, naamini watajitokeza kwa wingi Jumapili hivyo ni jukumu letu kuhakikisha wanafurahi,” amesema Pablo” amesema Pablo.

Vile vile kocha Pablo ambae ni raia wa Hispania ameongeza kuwa lengo la kwanza ni kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo ambao ni kama fainali kwao , lakini pia kuonyesha kandanda safi la kuvutia mashabiki watakaojitokeza.

Kikosi cha Simba kilingia kambini tangu juzi mchana na kuanza rasmi kufanya mazoezi jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo.

SOMA NA HII  KAMA UNA MTOTO MDOGO...HILI LA DStv LINAKUHUSU...ALADDIN INAKUJIA KWAKO KWA MSELELEKO ULE ULE WA MAMBO MOTO...