Home Habari za michezo RASMI…’FEI TOTO’ APIGWA ‘STOP’ KUCHEZA MPIRA…MADAKTARI WAMPA ONYO..ASIPOZINGATIA IMEKULA KWAKE…

RASMI…’FEI TOTO’ APIGWA ‘STOP’ KUCHEZA MPIRA…MADAKTARI WAMPA ONYO..ASIPOZINGATIA IMEKULA KWAKE…


JOPO la madaktari wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, limemtaka kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuhakikisha anapata mapumziko kamili ya kipindi kisichopungua mwezi mmoja, ili kuhakikisha anapona majeraha ya misuli aliyoyapata.

Fei Toto alipata majeraha hayo katika mazoezi ya kikosi cha Taifa Stars iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Sudani, ambao ulitarajiwa kupigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Nyota huyo wa Yanga alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Meneja wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema: “Feisal alipata majeraha wakati tukiendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Sudan, ambapo kutokana na ukubwa wa jeraha lake madaktari walimshauri apate mapumziko yasiyopungua mwezi mmoja. “Kutokana na umuhimu wa mapumziko hayo, hajapewa programu yoyote ya mazoezi kwani kwa kufanya hivyo inawezekana akaongeza ukubwa wa jeraha alilonalo.”

SOMA NA HII  JE, YANGA NA SIMBA KUTOSHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO ?