Home Uncategorized IHEFU YAISHUSHA MAZIMA MBAO FC LIGI DARAJA LA KWANZA, MBEYA CITY BADO...

IHEFU YAISHUSHA MAZIMA MBAO FC LIGI DARAJA LA KWANZA, MBEYA CITY BADO WAPOWAPO


LEO Agosti Mosi, Klabu ya Ihefu ya Mbeya imefanikiwa kupanda rasmi ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuishusha chini jumlajumla Klabu ya Mbao FC.

Ushindi walioupata Mbao wa mabao  4-2 mbele ya Ihefu SC umeshindwa kuibakisha timu hiyo inayonolewa na Felix Mizniro kubaki ndani ya ligi.

Mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Kirumba ulikuwa ni wa pili baada ya ule wa kwanza uliochezwa Mbeya, Mbao FC kukubali kichapo cha mabao 2-0 hivyo leo wameshshwa kwa faida ya mabao ya ugenini ambayo Ihefu wameshinda.

Kwa kuwa jumla inakuwa ni mabao 4-4 hivyo Mbao walipaswa washinde mabao matano ili kujihakikshia nafasi ya kubaki ndani ya ligi jambo ambalo limekuwa gumu kwao.

 Mabao ya leo kwa upande wa Mbao FC yalifungwa na mshambuliaji wao namba moja Wazir Junior ambaye ni nahodha pia dakika ya 7 na 45 mengine yalifungwa na Michael Masinda dakika ya 46 aliyejifunga na Datus Peter alifunga dakika ya 90+3 kwa penalti.

Kwa upande wa Ihefu mabao yalipachikwa na Joseph Kinyozi dakika ya 41 na lile walilomaliza kazi lilifungwa na Willy Mgaya dakika ya 88.

 Ihefu Sports Club inakuwa timu ya kwanza ya Ligi Daraja la Kwanza kupanda ligi kuu tangu mfumo wa Playoff uanze Tanzania.

Kwa upande wa mchezo wa Mbeya City dhidi ya Geita Gold leo, Mbeya City imefanikiwa kubaki Ligi kuu msimu ujao kwa ushindi wa bao 1-0 na kufanya wafungane jumla ya mabao 2-1 kwa kuwa mchezo wa kwanza ngoma ilikuwa ni 1-1.

 Hivyo basi jumla ya timu tano kutoka ndani ya ligi zimeshuka jumlajumla zitashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2020/21 ambazo ni Singida United, Alliance FC, Lipuli, Mbao FC na Ndanda.

SOMA NA HII  YANGA WAAENDELEA KUIVUTIA KASI RAYON SPORTS