Home Uncategorized SIMBA KWENYE LIGI KUU BARA WAMEKUMBUKA HIKI HAPA

SIMBA KWENYE LIGI KUU BARA WAMEKUMBUKA HIKI HAPA


PASCAL Wawa, beki kisiki ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa kwa sasa miongoni mwa vitu ambavyo anavikumbuka ni mpira ule wa ushindani.

Ligi Kuu Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaitikisa dunia kwa sasa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi binafsi huku akiukumbuka mpira wa ushindani.

“Mimi nimeukumbuka mpira kwa sasa kwani nimekaa muda mrefu bila kucheza ninaamini hali ikiwa sawa mambo yatarejea nasi tutaendelea kupambana.

“Kutokana na kauli ya Rais (John Magufuli) kuwa anafikiria kurejesha ligi limenifanya nifurahi nina amini tutarejea uwanjani hivi karibuni,” amesema.

Simba ikiwa imefunga mabao 63 Wawa ametoa pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA MTIBWA SUGAR