Home Uncategorized MASHINE HIZI TANO ZAWEKWA KWENYE RADA KUMALIZA TATIZO LA UBUTU WA USHAMBULIAJI...

MASHINE HIZI TANO ZAWEKWA KWENYE RADA KUMALIZA TATIZO LA UBUTU WA USHAMBULIAJI NDANI YA YANGA


MABOSI wa Yanga mkononi wana majina zaidi ya matano ya washambuliaji ambao wanawahitaji kwa msimu ujao kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Miongoni mwa majina hayo ambayo mabosi wa Yanga wanayajadili kwa ajili ya kuwasajili ni Mghana, Michael Sarpong na Mkongomani, Heritier Makambo. Pia lipo jina la Bigirimana Blaise na Relliants Lusajo wote wanakipiga ndani ya Namungo pamoja na Paul Nonga wa Lipuli.

Yanga hesabu zake ni kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikisuasua kwenye utupiaji wa mabao.

Ikiwa imecheza mechi 27 kibindoni imejikusanyia mabao 31 huku kinara wake akiwa ni David Molinga mwenye mabao nane.

Lusajo na Blaise wamekuwa kwenye mwendelezo mzuri ambapo kwa pamoja wamefunga mabao 21 Lusajo akitupia 11 na Blaise mabao 10 huku Nonga pia akiwa na mabao 11.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa ni suala la kusubiri wakati ukifika kwa sasa mambo ya usajili muda wake bado.
SOMA NA HII  AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA NDANDA