Home Uncategorized ISHU YA WACHEZAJI WANAOPIGWA PANGA NDANI YA SIMBA IMEFIKIA HAPA

ISHU YA WACHEZAJI WANAOPIGWA PANGA NDANI YA SIMBA IMEFIKIA HAPA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa hauwezi kuwaweka wazi wachezaji ambao wataachwa kwa msimu ujao wa 2020/21 kwa kuwa bado ripoti haijafika mezani.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, ipo kwenye mchakato wa kuboresha kikosi chake huku ikielezwa kuwa itawapiga chini wachezaji walioshindwa kwenda na kasi ya kikosi hicho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa kwa sasa hawawezi kutaja idadi ya wachezaji watakaoachwa kwa kuwa hawajapata ripoti.

“Siwezi kusema ni wachezaji wangapi wataondoka kwa sasa kwani bado tuna mechi mkononi na wachezaji wote wanakitu chao ambacho wanacho uwanjani.

“Tuna muda wa kusubiri kisha mambo yakiwa sawa kila mmoja atajua nani ataondoka na nani atabaki ndani ya Simba,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 84 baada ya kucheza mechi 36.

SOMA NA HII  WAZIRI WA UTAMADUNI AWEKA UTABIRI WA KIBABE SIMBA, YANGA CAFCL