Home Habari za michezo BENCHIKHA APIGA STOP USAJILI WA CHARAMBA SIMBA….ISHU NZIMA ILIANZIA HAPA…

BENCHIKHA APIGA STOP USAJILI WA CHARAMBA SIMBA….ISHU NZIMA ILIANZIA HAPA…

Habari za Simba leo

Juzi Simba ilishusha jembe usiku mnene kutoka Zimbabwe lililopandishwa boti kwenda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 na juzi usiku jamaa alianza katika pambano dhidi ya APR lililohitimisha hatua ya makundi.

Sasa kama hujui, Mzimbabwe huyo, Michael Charamba alijua anakuja kusaini mkataba wa kuichezea Simba, lakini akakutana na kigingi kutoka kwa Kocha Abdelhak Benchikha aliyeshtukia kitu kwake na kutaka acheze kwanza ili amsome vizuri.

Habari za ndani kutoka Simba zinaeleza kocha huyo aliwaambia mabosi, nyota huyo kutoka Chicken Inn apelekwe haraka Unguja ili awahi mechi hiyo ya APR ili kuona uwezo wake akihofia ‘kuuziwa mbuzi kwenye gunia’ kisha ndipo ampe mkataba.

Charamba anayemudu nafasi nne tofauti uwanjani alilazimika kucheza mchezo huo uliomalizika kwa suluhu na Benchikha aliutumia kumsoma kuona kama anastahili kupewa mkataba au la.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kinada kuwa jamaa ana nafasi ndogo kusainishwa, tofauti na ilivyokuwa kwa Babacar Sarr  aliyetambulishwa jana mchana akisainishwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo aliyemkaba Cristiano Ronaldo ametua Simba kama mchezaji huru baada ya kuachana na US Monastir akiwa ni mchezaji wa kwanza wa kigeni kutambulishwa, huku nyota wengine wawili Ladeck Chasambi (Mtibwa Sugar) na Edwin Balua (Tanzania Prisons) watatambulishwa muda wowote kuanzia sasa.

“Ni kweli Simba inataka kumsajili Charamba, lakini kocha alisema kabisa kabla ya hajasaini mkataba anataka kwanza kumuangalia akiona anafaa basi atapewa mkataba na si vinginevyo. Ndio maana tumempeleka Zanzibar kuwahi mechi ya APR. Kwa sasa Simba tumekamilisha sajili nne tu,” kilisema chanzo kilichoomba hifadhi ya jina.

“Tumepokea mapendekezo ya kocha na tunayafanyia kazi, Benchikha ndiye atakayeamua kama anamfaa ama la baada ya kumuangalia.”

KIUNGO MSENEGALI

Mapema jana mchana Simba ilimtambulisha kiungo Msenegali Babacar Sarr akiwahi kumkaba CR7 wa Al Nassr ya Saudia katika mechi ya Klabu Bingwa kwa timu za Kirabuni akiwa na US Monastir ya Tunisia aliyoachana nayo Novemba mwaka jana. Habari zinasema Sarr kapewa miaka miwili akiwa ni nyota wa pili kutambulishwa na Simba baada ya kiungo Saleh Karabaka kutoka JKU.

SOMA NA HII  MZIZE KUONDOKA YANGA...TIMU HII YA EPL YAWANIA SAINI YAKE...ZAHERA AINGILIA KATI