Home Habari za michezo SIKU YA KWANZA KAZINI AKIWA NA SIMBA…BENCHIKHA AMPIGA MKWARA WA KUFA MTU...

SIKU YA KWANZA KAZINI AKIWA NA SIMBA…BENCHIKHA AMPIGA MKWARA WA KUFA MTU CHAMA…

Habari za Simba

KOCHA mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ameanza kuonyesha makucha yake na kusema hatoangalia ukubwa wa jina la mchezaji au kipenzi cha nani zaidi ya kutaka kuona kiwango bora na kupambania klabu hiyo kufikia malengo.

Itafahamika kuwa Chama ndiye kipenzi cha mashabiki wengi wa Simba huku akiwa pia na ushawishi kwa wachezaji wenzake, hivyo mkwara wa Bencikha kwa namna moja au nyingine yeye pia anahusika.

Kocha huyo alisema malengo yao ni kufanya vizuri lazima mchezaji anatakiwa kupambana na sio kujiona mkubwa ndani ya timu kwa sababu malengo lake kubwa ni kuifanya timu hiyo kupata ushindi uwanjani na kutwaa mataji mbalimbali ya ligi ya ndani na kufikia malengo katika michuano ya kimataifa.

Alisema ili timu kupata mafanikio lazima kuwepo kwa mshikamano baina ya timu, viongozi na mashabiki kwa ujumla, mashabiki wanatakiwa kusapoti timu yao.

“Kuna vingi navijua nimekuja na mikakati yake na atapata nafasi ya kuona wachezaji wake na kuangalia yupi anamfaa au hamfai. suala la mashindano ninaimani nitafanikiwa kufanya vizuri kwa sababu mimi ni mpambanaji,” alisema Benchikha.

Aliongeza kuwa anaimani atawafurahisha mashabiki kwa kutengeneza Simba mpya na imara kikubwa anahitaji sapoti na ushirikiano mkubwa kutoka kwao na kufanikisha kile ambacho wanakitarajia.

Kocha huyo alisema amekuja kwa malengo ya kufanikiwa kwa klabu ya Simba kama ilivyo kwa klabu alizotoka kubwa zaidi ni ushirikiano mkubwa hasa kwa

Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula alisema wametamatisha shauku ya mashabiki kumpta mwalimu, walipokea wasifu nyingi kutoka kwa makocha mbalimbali lakini walikuwa na kipindi kigumu kupata kocha mzuri kama ilivyo kwa Benchikha.

“Benchikha atakuwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili, atamalizia msimu huu na msimu ujao, mashabiki wanatakiwa kuwa watulivu kwa sababu kocha mpya, viongozi tumempa uhuru wa kufanya kazi na hatuna utaratibu wa kumpangia kocha kupanga kikosi nani acheze na asicheze,” alisema Kajula.

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA KAMILI NA TEREHE KWA MECHI ZA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA...