Home news MO DEWJI – MAFANIKO SIO KITU CHEPESI…NILITAKA UBINGWA AFRIKA…AFUNGUKA USAJILI WA ADEBAYO…

MO DEWJI – MAFANIKO SIO KITU CHEPESI…NILITAKA UBINGWA AFRIKA…AFUNGUKA USAJILI WA ADEBAYO…


RAIS wa Heshima wa Klabu ya Simba, MohamedDewji amesema kuwa wana imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane.

Jumapili,  Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya RS Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mo amesema:-“Shabaha yangu ilikuwa katika miaka 10 tuweze kuchukua ubingwa katika mashindano ya kimataifa lakini haijawa hivyo bado tuna nafasi ya kufanya vizuri.

“Kupoteza mbele ya RS Berkane haitupi presha kwa sababu tuliwahi kufungwa na Al Ahly mabao 5 na AS Vita walitufunga mabao 5 lakini tuliweza kutinga hatua ya makundi.

“Mafanikio siyo kitu chepesi kuna hatua na sisi tunataka kuwa bora. Kwa upande wa usajili tutajipanga na watu wetu wa kufuatilia wachezaji wapo tayari kukamilisha usajili.

“Adebayo huyu pia ni mchezaji mzuri nilipigiwa simu na viongozi wa Simba tutazungumza nao hivyo ni jambo ambalo lipo tusubiri na tuone,”.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUA MISRI...LUIS AFUNGUKA HAYA KUHUSU PENGO LAKE SIMBA..AWATAJA VIONGOZI