Home Habari za michezo HAWA HAPA MASTAA WANNE WALIOTEMWA TAIFA STARS KIKOSI CHA MWISHO AFCON 2023…

HAWA HAPA MASTAA WANNE WALIOTEMWA TAIFA STARS KIKOSI CHA MWISHO AFCON 2023…

Taifa Stars leo

Kipa Metacha Mnata na mshambuliaji Abdul Selemani ‘Sopu’ ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Taifa Stars ambao hawajajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu huko Ivory Coast.

Kwa mujibu wa orodha ya vikosi vya timu zote 24 zitakazoshiriki fainali hizo iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Sopu anayechezea Azam na Metacha wa Yanga, hawamo katika majina ya wachezaji 27 walioorodheshwa katika kikosi cha mwisho cha Taifa Stars.

Mbali na Sopu na Metacha, wengine wawili ni Khleffin Hamdoun na Twariq Yusuf.

Wanne hao walikuwa miongoni mwa wachezaji 31 wa Taifa Stars ambao wapo kambini kujiandaa na fainali hizo lakini kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya Afcon, idadi ya wachezaji wanaohitajika kikosini ni 27.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA USAJILI WA PHIRI...MWAKALEBELA AAMUA KUIWAHI SIMBA ...AGUSIA MCHEZO MZIMA ULIVYO...