Home Habari za michezo WAKATI WATU WAKIHISI PENGINE NI MORRISON..SENZO AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUTEMANA NA...

WAKATI WATU WAKIHISI PENGINE NI MORRISON..SENZO AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUTEMANA NA YANGA…ADAI HAKUWA NA JINSI ZAIDI YA KUFANYA HIVYO…


Saa chache baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kwamba aliyekuwa Ofisa Mtendaji wao Mkuu Senzo Mazingiza anaondoka mwenyewe ameibuka na kukanusha juu ya kuondoka kwake kuhusishwa na ujio wa mshambuliaji Bernard Morrison.

Akizungumzia ishu ya kupishana mara mbili na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison Senzo amesema wala hana tatizo na usajili huo na kwamba alihusika mara zote kumsajili Mghana huyo katika klabu zote.

“Niliwahi kuwaambia ninyi Mwanaspoti juu ya Morrison, bahati mbaya hapa Tanzania uongo hupewa nafasi kubwa kusambaa, nilisema nilipokuwa Simba nilihusika kumleta Morrison pale lakini bahati mbaya wakati anafika mimi nilikuwa naondoka,” amesema Senzo

“Nikiwa hapa Yanga pia imekuwa hivyohivyo, viongozi wenzangu wanajua jinsi tulivyoshirikiana kumleta huyu Morrison, huyu ni mchezaji bora bila kuangalia mambo yake yanayosemwa.

“Nina imani kubwa Morrison atakwenda kuwafanyia kazi kubwa wananchi ambao wamempokea tena bila kinyongo, hata mimi nitafarijika nikisikia Morrison akiwa anafanya kazi bora hapa.

“Mimi bado ni mwananchi hapa nitaendelea kuwasailiana na viongozi wenzangu, sijaondoka Yanga kwa ubaya kabisa ndio maana mmekuwa mkiniona hapa katika kazi zote, bahati mabya hili lilitakiwa niliamue sasa wakati ambao pia mkataba ulikuwa unakwisha.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA NAMNA VIONGOZI 'WANAVYOMHENDO'...AANIKA MAKUBALIANO YOTE...