Home Uncategorized MAURIZIO SARRI ATIMKA CHELSEA AIBUKIA JUVENTUS

MAURIZIO SARRI ATIMKA CHELSEA AIBUKIA JUVENTUS


MAURIZIO Sarri aliyekuwa meneja wa Chelsea sasa ni mali ya Juventus ambapo amesaini kandarasi ya miaka mitatu.

Timu yake ya zamani Chelsea imethibitisha kocha wake Sarri kusepa katika timu hiyo na kutua Juventus.
Juventus, wamemtangaza Sarri kuwa meneja wao mpya, akichukua mikoba ya Max Allegri, aliyeachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.

Sarri amedumu kwenye kikosi cha Chelsea kwa miezi 11 huko Stamford Bridge, akiwaongoza kubeba ubingwa wa Europa Ligi na kuwarudisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.
SOMA NA HII  KLOPP ACHEKELEA KUITUNGUA ARSENAL MABAO 3-1