Home Uncategorized KABUNDA AFUNGA BAO LA KIDEO WAKATI YANGA IKILALA KWA MABAO 3-0

KABUNDA AFUNGA BAO LA KIDEO WAKATI YANGA IKILALA KWA MABAO 3-0

HASSAN Kabunda, winga wa KMC leo alimaliza msumari wake wa mwisho kwa kumtungua mlinda mlango wa Yanga bao la kideo kwa mpira wa adhabu uliomshinda Metacha Mnata wakati Yanga ikikubali kulala kwa mabao 3-0.

Mchezo wa leo wa kirafiki ulichezwa ulichezwa Uwanja wa Uhuru ambapo ushindani ulikuwa mkubwa kwa timu zote mbili.

KMC ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Sadala Lipangile dakika ya 31 kwa pasi ya Charlse Ilanfya na bao la pili likapachikwa na Ilanfya kwa pasi ya Emmanuel Mvuyekule.

Mchezo unaofuata wa Yanga utakuwa dhidi ya Mwadui ambao utakuwa ni wa Ligi Kuu Bara inayoendelea mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  KIPIGO WALICHOPOKEA YANGA CHA MABAO 3-0 MBELE YA KMC NI FAIDA KWAO