Home Uncategorized MAWAZO YA CHAMA YEYE NI USHINDANI TU

MAWAZO YA CHAMA YEYE NI USHINDANI TU


CLATOUS Chama, kiungo wa Simba amesema kuwa anaamini ushindani utakuwa mkubwa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kila timu kujipanga kupata ushindi.

Chama amerejea leo na ndege ya kampuni ya Ethiopia akitokea nchini Zambia ambapo alikuwa kwa ajili ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.

 Nyota huyo kipenzi cha mashabiki amesema:-“Ushindani utakuwa mkubwa na kila timu inahitaji ushindi jambo ambalo linatufanya nasi tujue kwamba tuna kazi ngumu ya kufanya.

“Ninafurahi kwa kuwa nimerejea, nitakachofanya ni kuongeza juhudi na kushirikiana na wachezaji wenzagu ili kushinda mechi zetu zilizobaki.”

Simba ikiwa imefunga mabao 63, Chama amehusika kwenye mabao tisa.

SOMA NA HII  MFAHAMU VIZURI SHIBOUB ALIPOZALIWA MPAKA ANATUA SIMBA - VIDEO