Home Habari za michezo KISA KUPIGWA KIZEMBE NA WASUDAN…SALEH JEMBE NAYE AWAPA ZA USO YANGA SC….

KISA KUPIGWA KIZEMBE NA WASUDAN…SALEH JEMBE NAYE AWAPA ZA USO YANGA SC….

Mchambuzi wa soka nchini, Saleh Ally ‘Jembe’ amesema ni wakati sasa kwa Timu ya Yanga kufanyia kazi nafasi wanazotengeneza hasa katika mashindano ya kimataifa kwa sababu nafasi za kufunga huwa zinakuwa chache.

Baada ya kutolewa na Al Hilal ya Sudan kwenye ligi ya Mabingwa Afrika nakuangukia kwenye Kombe la Shirikisho na wamepangwa kucheza na Club Africain ya Tunisia Novemba 2, 2022 uwanja wa Benjamin Mkapa Dar.

Katika michezo yote minne ya hatua ya awali, kuanzia dhidi ya Zalan FC kisha Al Hilal, Yanga wameonekana kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini wanashindwa kuzitumia nafasi hivyo ipasavyo jambo ambalo limewagharimu na kusababisha kufungwa na kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa.

SOMA NA HII  SAKHO NAYE ANYOOSHA MIKONO SIMBA...WAKALA WAKE AGUNGUKA A-Z...AZAM FC WAHUSISHWA..