Home Uncategorized SIMBA YAWEKA MEZANI MILIONI 10 KWA AJILI YA KELVIN YONDAN, METACHA MNATA,...

SIMBA YAWEKA MEZANI MILIONI 10 KWA AJILI YA KELVIN YONDAN, METACHA MNATA, JUMA KASEJA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa endapo timu ya Taifa ya Tanzania itaibuka kidedea mbele ya timu ya Kenya leo watapewa zawadi ya milioni 10.

Zawadi hizo zitakuwa ni kwa timu nzima kwa ajili ya pongezi ambayo imelenga kuwapa morali wachezaji hao ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa leo wa kufuzu Chan utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Kupita kwenye ukurasa wa Instagram wa Simba taarifa iliandikwa kuwa ahadi hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori kwa niaba ya Simba.

Miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa ni pamoja na Kelvin Yondan, Metacha Mnata, Paul Godfrey, Aish Manula, Juma Kaseja, Erasto Nyoni na Ibrahim Ajib ambao mkwanja huo wa milioni 10 unawahusu.

SOMA NA HII  NYOTA STARS: INAWEZEKANA KUPATA USHINDI LEO MBELE YA KENYA