Home Uncategorized ZUBER KATWILA: WACHEZAJI NIMEWAPA PROGRAM MAALUM

ZUBER KATWILA: WACHEZAJI NIMEWAPA PROGRAM MAALUM

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wachezaji wamepewa kazi kubwa ya kuwa mabalozi kwenye familia zao na kujilinda na Virusi vya Corona.

Kwa sasa wachezaji wa Mtibwa Sugar wamevunja kambi na kila mchezaji anafanyia mazoezi yake nyumbani akiwa na familia yake baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa amewapa wachezaji wake program na anawasiliana nao ili kujua wanatimiza namna gani kazi waliyopewa.

“Hakuna wachezaji waliopo kambini kwa sasa tumewaruhusu waelekee nyumbani na kufanya mazoezi wakiwa na program ambazo zitawafanya wazidi kuwa bora.

“Ninaona kabisa bado tunawafuatilia kwa ukaribu na kila mmoja anatimiza kile ambacho amepewa, pia tumewaelekeza wawe makini kujilinda na Virusi vya Corona kwa kuwa mabalozi wazuri nyumbani, ” amesema Katwila.

SOMA NA HII  UNAWEZA KUMALIZA JUMAPILI BILA KUKUBASHIRI NA MERIDIAN BET