Home Uncategorized MO RASHID SASA DOZI YAKE NI KUTWA MARA MBILI

MO RASHID SASA DOZI YAKE NI KUTWA MARA MBILI


MOHAMED Rashid,’Mo Rashid’ nyota anayekipiga ndani ya JKT Tanzania kwa mkopo akitokea Klabu ya Simba amesema kuwa kwa sasa anapiga dozi ya mazoezi mara mbili kwa siku ili kulinda kipaji chake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Rashid amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi asubuhi na jioni kwa kufuata program alizopewa na Kocha Mkuu, Mohamed Abdallah.

“Nipo nyumbani kwa sasa nikiendelea na mazoezi pia ninaomba dua ili hali ikae sawa maana hapa kwa sasa mambo bado hayajakaa vizuri.

“Bado kuna ugumu ambao upo kutokana na kukosa uhuru ambao tulikuwa nao mwanzo lakini hilo halina maana kwamba tupuuzie masuala ya kanuni haitapendeza,” amesema Rashid.

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SABABU YA KUTUMIA BASI KUIFUATA JKT TANZANIA