Home Uncategorized NIYONZIMA AWAPA SOMO HILI WACHEZAJI

NIYONZIMA AWAPA SOMO HILI WACHEZAJI

HARUNA Niyozima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa ni busara kwa wachezaji kufanya mazoezi wakati huu wa mapumziko na kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.

Niyonzima amekuwa kwenye ubora wake msimu huu baada ya kurejea ndani ya Yanga licha ya kutumia muda mfupi amepata nafasi kikosi cha kwanza baada ya kujiunga na klabu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo akitoa AS Kigali ya Rwanda.

Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa:”Ni muhimu kwa kila mchezaji kufanya mazoezi akiwa nyumbani na kuchukua tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona.

“Ubora wa mchezaji unabebwa na mazoezi pamoja na kujituma bila kuchoka, jambo la kuzingatia pia kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona,”.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA BETIKA, JIPATIE NAKALA YAKO NI BURE