Home Uncategorized DUH! SHILOLE KWA FIKSI BALAA, ETI HAJAWAHI KUGUSWA

DUH! SHILOLE KWA FIKSI BALAA, ETI HAJAWAHI KUGUSWA

MUME wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ Ashiraf Uchebe, amesema tangu aanze kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo mpaka anamuoa hajawahi kumpiga hata kofi.
Uchebe ameibuka na maelezo hayo baada ya kuwepo kwa madai ya muda mrefu mitandaoni kuwa amekuwa na kawaida ya kumwangushia kipondo mkewe huyo.
Akizungumza na MIKITO Uchebe alisema watu wengi wanamuona kama baunsa ambaye kila wakati anaweza kupiga mtu, kitu ambacho si kweli kwani anampenda sana mkewe huyo na kamwe hawezi kumgusa.

“Watu wengi wananichukulia tofauti sana wananiona kama mtu wa kupiga kila wakati lakini siyo kweli kabisa, sijawahi kumpiga mke wangu hata mara moja na sitaweza kufanya hivyo,” alisema Uchebe.
Kwa upande wa Shilole, alipoulizwa kuhusu maelezo hayo, alisema ni kweli, tangu aolewe na Uchebe hajawahi kumgusa. “Sijui wanamuonaje mume wangu au kwa sababu kajazia ndiyo maana wanasema ananipiga, yaani kiufupi hajawahi kunigusa kabisa,” alisema Shilole.
SOMA NA HII  STARS YAPEWA RAI YA KUCHUKUA KIKOMBE MISRI, LAZIMA IFUATWE