Home Uncategorized SASA SIMBA WAHAMISHIA HASIRA MCHEZO WA MARUDIO KIMATAIFA, WAWAITA MASHABIKI

SASA SIMBA WAHAMISHIA HASIRA MCHEZO WA MARUDIO KIMATAIFA, WAWAITA MASHABIKI


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mpango mkubwa wa kikosi chake ni kwenye mchezo wa marudio dhidi ya UD Songo

Simba jana ilicheza mchezo wa kwanza wa kimataifa kwenye hatua ya awali dhidi ya UD Songo, uwanja wa Beira nchini Msumbiji mpaka dakika 90 kukamilika ubao ulikuwa unasoma 0 kwa UD Songo na Simba pia.

Baada ya kumaliza mchezo huo kikosi kilikwea pipa na leo kipo Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC utakaochezwa Jumamosi.

“Tumerudi salama ni jambo la kushukuru, kwa sasa kazi kubwa ni kuelekea kwenye mchezo wetu wa marudio ambao tutakuwa nyumbani hivyo mashabiki wajitokeze kutupatia sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  JESHI LA KAZI LA YANGA LEO DHIDI YA LIPULI