Home Uncategorized SINGIDA UNITED YAJICHIMBIA MWANZA

SINGIDA UNITED YAJICHIMBIA MWANZA


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kwa sasa unaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 23.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa timu imejichimbia Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.

“Timu kwa sasa ipo Mwanza inaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea Ligi Kuu Bara, kazi bado inaendelea.

“Kocha, Felix Minziro anasuka kikosi cha ushindani ambacho kitafanya vema ligi itakapoanza hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  HIVI HAPA VIGONGO VITATU VYA AZAM FC JUNI