Home Habari za michezo HAYO MAPOKEZI YA MAYELE HUKO MISRI, SIO POA UNAAMBIWA KAMA MFALME

HAYO MAPOKEZI YA MAYELE HUKO MISRI, SIO POA UNAAMBIWA KAMA MFALME

MAYELE ATOBOA SIRI ZA MAZEMBE...KOCHA YANGA ALIMTUMA MISHENI YA SIRI

SASA ni rasmi kuwa nyota wa Yanga raia wa DR Congo, Fiston Mayele ameondoka rasmi klabuni hapo kwenda nchini Misri kwa ajili ya kujiunga na Klabu ya Pyramids huku nyuma Yanga nao wamemshusha mbadala wake ambaye ni raia wa Cameroon, Emmanuel Mahop.

Mayele ambaye alijiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea AS Vita ya nchini kwao, anaondoka Yanga baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita akifunga mabao 17 sawa na Said Ntibazonkiza wa Simba.

Mayele aliondoka nchini Alhamisi saa 8 usiku na Shirika la Ndege la Qatar akiwa na meneja wake, Jasmin ambapo wamekwenda kusaini mkataba rasmi baada ya kufikia makubaliano ya pande zote kati ya Yanga na Pyramids na mchezaji mwenyewe.

Mmoja wa watu wa karibu wa Mayele aliliambia gazeti hili kuwa, straika huyo ameandaliwa mapokezi ya kipekee sambamba na kuwekwa kwenye hoteli ya nyota tano huko Misri wakati akisubiri kusaini rasmi.

Championi Ijumaa lilimshuhudia Mayele usiku wa kuamkia jana Alhamisi, akiwa na meneja wake, Jasmin pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akisepa zake kwenda Misri, huku mshambuliaji huyo akiwataka mashabiki wa Yanga kutohuzunishwa na kuondoka kwake.

“Mayele ameondoka ila amewataka mashabiki wa Yanga kutohuzunishwa na hilo na badala yake anaamini watapata straika bora atakayekuja kuziba nafasi yake na kuwafikisha kwenye hatua kubwa kimataifa,” alisema mmoja wa mameneja wake.

UJIO WA STRAIKA MPYA
Baada ya Mayele kusepa rasmi, sasa unaambiwa muda wowote kuanzia sasa Yanga watamtambulisha Mahop ambaye tayari ameshatua nchini.

Mahop alitarajiwa kutua nchini usiku wa kuamkia jana Alhamisi akitokea kwao baada ya Yanga kumalizana na uongozi wake.

Chanzo chetu cha uhakika kutoka Yanga kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, Yanga wamelazimika kumalizana na Mahop baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya rekodi za Sudi Abdallah raia wa Burundi waliyekuwa wakimtaka mwanzo.

Kiliongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa akatambulishwa kabla ya Mayele kutambulishwa kwenye klabu yake mpya ya Pyramids ya huko Misri.

“Yanga wanategemea leo (jana), Alhamisi kumpokea straika wao mpya raia wa Cameroon ili wamtambulishe kabla ya utambulisho wa Mayele huko Misri ambaye wanaamini kama atatambulishwa kabla yao basi hali itachafuka sana.

“Muda wowote leo (jana) watamtangaza Mahop mara baada ya kumsainisha mikataba ambapo wamempatia miaka miwili,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

SOMA NA HII  SIMBA IPO SIRIAZI KIASI HICHI...OUATTARA AONDOLEWA KAMBINI...SAWADOGO AREJEA MAZOEZINI