Home Habari za michezo YANGA WAANZA NA TUNZO MAPEMAAAAAA, HAPA GAMONDI PALE NZEGELI

YANGA WAANZA NA TUNZO MAPEMAAAAAA, HAPA GAMONDI PALE NZEGELI

Habari za Yanga

NYOTA wa Yanga, Maxi Nzengeli, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Agosti katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24, huku Miguel Gamondi wa Yanga, akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Nzengeli amewashinda Aziz Ki wa Yanga na Jean Baleke wa Simba alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kwa mwezi huo, Nzengeli alifunga mabao mawili, akisaidia upatikanaji wa bao moja

Kwa upande wa Gamondi, aliwashinda Roberto Oliveira wa Simba na Hemed Morocco wa Geita, ambapo kwa mwezi huo Yanga iliifunga KMC mabao 5-0, kisha ikaifunga JKT Tanzania idadi kama hiyo ya mabao. Timu zote zilicheza michezo miwili mwezi huo.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, Godfrey Komba kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Agosti, kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

SOMA NA HII  KOCHA MJERUMANI AANDALIWA MIKOBA SIMBA...KUTANGAZWA FASTA ..KUANZA NA WAZAMBIA..CHAMPION