Home Azam FC DUBE ANAITAKA TUZO YA UFUNGAJI BORA BONGO

DUBE ANAITAKA TUZO YA UFUNGAJI BORA BONGO


 MSHAMBULIAJI tegemeo ndani ya kikosi cha Azam FC, Prince Dube raia wa Zimbabwe amesema atazidi kupambania ndoto zake za kuwa mfungaji bora msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.

 

Dube ameyasema hayo baada ya kufikisha mabao 12 na kuwa kinara akimzidi bao moja Meddie Kagere wa Simba.

 

Kwa misimu miwili mfululizo, Kagere amefanikiwa kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora katika Ligi Kuu Bara na msimu huu anaifukuzia kwa mara ya tatu.


Kwa sasa Kagere ndani ya Simba ametupia mabao 11 anafuatiwa na John Bocco mwenye mabao 10 kibindoni.


Dube amesema: “Nawashukuru wachezaji wenzangu kwani mara zote wamekuwa wakinipa nafasi mimi ya kufunga na kunisogeza karibu na ndoto zangu.

 

“Ni ndoto yangu kuwa mfungaji bora ila nikiikosa basi nitahakikisha naisaidia timu yangu kufanya vizuri kwa kila mechi na nitakapopata nafasi ya kufunga basi nitaitumia vizuri,” .

Bao la 12 la Dube alifunga Uwanja wa Mkapa mbele ya Yanga kwa kumtungua Faroukh Shikalo akiwa nje ya 18.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA