Home Yanga SC YANGA WATUMA UJUMBE KMC, YAWAKUMBUSHA KWAMBA WANAONGOZA LIGI

YANGA WATUMA UJUMBE KMC, YAWAKUMBUSHA KWAMBA WANAONGOZA LIGI

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 10.

Kwenye msimamo Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 inafuatiwa na watani zao wa jadi Simba wenye pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

Wapinzani wao KMC kwenye msimamo wapo nafasi ya tano na pointi zao kibindoni ni 35 na wamecheza jumla ya mechi 24.

Kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba, KMC iliyeyusha pointi zote tatu mazima kwa ubao kusoma KMC 1-2 Yanga hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kazi kubwa ambayo ipo kwa wachezaji ni kusaka ushindi kwenye mechi zao ambazo watacheza ili kupata pointi tatu.

“Maandalizi yapo sawa na ninapenda kuwaambia mashabiki kwamba wasiwe na mashaka sisi ni Yanga na tunahitaji kuonyesha kwamba tupo vizuri.

“Mashabiki wasisahau kwamba tunaongoza ligi hivyo wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kushuhudia namna tutakavyofanya mbele ya KMC, tunaamini utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani ila tupo tayari,” .

Baada ya kuchimbishwa kwa Cedric Kaze kwenye benchi la ufundi nafasi yake ipo mikononi mwa Juma Mwmabusi ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo iliyoweka kambi Kigamboni.

                             

SOMA NA HII  MUSONDA APELEKA SHANGWE JANGWANI, ATHIBITISHA KUWA YEYE NI MWAMBA