Home Habari za michezo STRAIKA MWILI NYUMBA ANUKIA SIMBA SC…JAMAA ANATUPIA HUYOO….

STRAIKA MWILI NYUMBA ANUKIA SIMBA SC…JAMAA ANATUPIA HUYOO….

Marou to Simba SC

Baada ya juzi kumtambulisha Saido Ntibazonkiza kutoka Geita Gold, kisha kumuongezea mkataba, beki Henock Inonga aliyekuwa akinyemelewa na Azam FC, mabosi wa Simba  SC wameendelea kuwapa raha mashabiki kwa kujiandaa kumshusha straika kutoka Cameroon, Souaibou Marou.

Inonga ameongezwa mkataba wa miaka miwili utakaomalizika 2025 na kufuta ndoto za Azam iliyokuwa ikimpiga hesabu, lakini mezani kwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ kuna majina ya mastraika wa maana wawili wakipigiwa ana ana doo, ili mmoja atue Msimbazi katika dirisha dogo.

Ukiacha jina la mshambuliaji wa USM Alger anayecheza kwa mkopo Najran, Kwame Opoku, pia Simba ina jina la Marou anayekiopiga Coton Sport ya Cameroon pamoja na timu ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Try Again kwa dili la Opoku amemtumia wakala aliyemleta, Nelson Okwa kutoka Nigeria na tayari amekamilisha kila kitu kama ambavyo alikuwa anahitaji ili kumpata nyota huyo.

Simba SC imeambiwa na USM Alger itoe USD 30,000 zaidi ya Sh60 milioni ili kuvunja mkataba wa mwaka mmoja uliobaki na mchezaji ametaka USD 50,000 zaidi ya Sh100 milioni pesa ya usajili na mshahara ametaka USD 6000 zaidi ya Sh12 milioni atakayokuwa anavuta kila mwisho wa mwezi.

Baada ya mazungumzo hayo ya wakala wa Okwa, uongozi wa USM Alger na Opoku kukamilika ripoti yote amekabidhiwa Try Again na kazi imebaki kwake kumchukua Opuku au kufanya maamuzi mengine.

Ukiachana na mchakato huo wa Opuku kufikia hatua nzuri mezani kwa Try Again ana jina la Mcameroon Marou anayecheza pia timu ya taifa hilo.

Marou ameuvutia uongozi huo wa Simba hadi kutenga muda na kumuangalia na kumfuatilia straika huyo mwenye uwezo wa kufunga mabao aina mbalimbali, spidi, msumbufu kwa mabeki pamoja na sifa nyingine nyingi.

Hata hivyo, Simba ikiendelea kumfuatilia Marou inaweza kukutana na ugumu wa kumpata kwenye maeneo mawili bajeti ya kupatikana kwake pamoja na ofa nyingine kubwa aliyokuwa nayo kutokea Australia.

Alipoulizwa Try Again alisema Simba ipo sokoni kutafuta wachezaji wazuri kulingana na mapendekezo ya benchi lao la ufundi na malengo yao ni kusajili wachezaji ambao wataongeza ubora wa kikosi . “Tunahitaji wachezaji watakaoongeza ubora wa timu kwenye mashindano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ndio maana tunataka wale wazuri watakaocheza kwenye mashindano yote haya,” alisema Try Again.

INONGA HADI 2025

Katika hatua nyingine, mabosi wa Simba wamemaliza utata kwa beki Henock Inonga kwa kumpa mkataba wa miaka miwili hadi 2025 na kufuta ndoto za Azam kumbeba. Mkataba wa Inonga ulikuwa ukielekea ukingoni na Azam ilikuwa ikimtaka na Simba iliyoanza naye mazungumzo imemuongezea mkataba mpya.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHINDWA KUWIKA MSIMU HUU...CHAMA AWAANGUA SIMBA...UJUMBE WAKE HUU HAPA...