Home Habari za michezo KUELEKEA SIMBA vs AL AHLY KESHO KUTWA….UWANJA WA MKAPA KAMA ULAYA VILEEE….

KUELEKEA SIMBA vs AL AHLY KESHO KUTWA….UWANJA WA MKAPA KAMA ULAYA VILEEE….

Uwanja wa Mkapa

UWANJA wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, sasa umekamilika kwa asilimia 99 na tayari kwa ajili ya mechi ya ufunguzi rasmi wa mashindano ya Afrika Football League (AFL).

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Ijumaa hii kati ya Simba ambao ni wenyeji wakiwakaribisha Al Ahly ya Misri utakaopigwa uwanja huu, saa 12:00 jioni.

Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa, Milinde Mahona alisema awamu ya kwanza ya ukarabati wa uwanja umekamilika kwa asilimia kubwa na wanatarajia ndani ya siku chache kukamilika.

Alisema uwanja unafunguliwa rasmi kwa ajili ya michuano ya AFL na utaendelea kutumika katika michezo hiyo baada ya hapo utaendelea kufanyiwa marekebisho kwa awamu wa pili.

“Katika awamu wa pili utakuwa katika kufumua uwanja wa kuchezea na sehemu ya kukimbilia riadha, hiyo ni awamu ya pili kwa ajili ya kujiandaa na uwenyeji wa mashindano mbalimbali ikiwemo AFCON ya 2027.

Lakini kabla ya kufanya ukarabati wa awamu ya pili itafanywa tathimini baadae maamuzi yatatolewa kama Simba au Yanga kuweza kutumia uwanja huu katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Meneja huyo.

Aliongeza kuwa Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha ukarabati wa awamu ya pili unafanyika kwa haraka ili hizo klabu na timu za Taifa kuweza kutumia uwanja katika mashundano makubwa.

Kuhusu Changamoto za maji hasa vyooni, alisema  limefanyiwa kazi na halijirudii tena kwa sababu wamekuwa makini kufanyia maboresho kila sehemu ambayo ilikuwa na shida.

 “Sehemu ya waandishi  imetengwa na kufanyiwa maboresha  hawataingiliwa na mashabiki kama ilivyokuwa awali kwa sababu ni maalum kwa ajili kufanya kazi zao.

Hizo nazo zimefanyiwa kazi pia kikubwa mashabiki kuweka kufuata taratibu na kuingia uwanjani mapema kuepuka msongamano wa milangoni na mageti,” alisema Meneja.

Suala la viti kuwekwa namba na mashabiki kukaa sehemu husika, Mahona alisema kwa sasa Utaratibu utakuwa kama awali hadi hapo ukarabati wa awamu ya pili itakapofanyia tena.

“Nakiri awali kulikuwa na changamoto ya taa  umeme ukikatika, unaporejea inachukua dakika 25 hadi 15 kuwaka, sasa tumeboresha kwa kufungwa taa mpya kama itatokea changamoto zozote za umeme basi zitawaka kwa haraka sana.

Pia tumenunu Jenereta kwa ajili ya sehemu ya kucheza ya uwanja lakini tumezungumza na Shirika la Umeme (TANESCO) kusiwepo kwa mgao wa umeme,” alisema Mahona.

Alisema utaratibu shirikisho la soka taifa ambalo timu inahitaji kutumia uwanja itawasiliana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kupewa muongozo ambao wataandika barua kwa katibu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuangalia uwezekano wa siku hiyo kupatikana kwa uwanja.

Gharama za kukodi ni Mill 20, iwe timu zote za ndani au nje, mfano Simba au Yanga katika sherehe zao basi watatoa kiasi hicho iwemo mechi za ligi au kimataifa wanalazimika kutoa asilimia 15 ya mapato ya mechi,” alisema Meneja huyo wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  ZA NDAANI KABISAA....DILI LA MOSES PHIRI NA SIMBA NI TAREHE TU....PABLO HUMWAMBII KITU KWA MUGALU....