Home Habari za michezo KWISHA KAZI….VIGOGO WAZITO YANGA SC WAITIBULIA AZAM FC KWA FEI TOTO…

KWISHA KAZI….VIGOGO WAZITO YANGA SC WAITIBULIA AZAM FC KWA FEI TOTO…

Habari za Yanga

Kiungo fundi kutoka Visiwa vya Karafuu, Zanzibar anayekipiga katika Klabu ya Yanga Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amerejea rasmi katika kikosi cha timu hiyo baada ya sintofahamu ya siku kadhaa kati yake na waajiri wake hao.

Taarifa za awali zinadai kuwa Feisal Salum amerejea kikosini Yanga na wamekubaliana kukaa pamoja na kujadili kuhusu kuboresha maslahi ya mkataba wake ndani ya klabu hiyo ambayo kwa mujibu wa mkataba atawatumikia Wananchi mpaka mwaka 2024.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Yanga kimetuhakikishia kuwa “kila kitu kipo sawa kati yao”.

Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni ,Feisal aliandika barua na kuwaaga mashabiki na wapenzi wa Yanga huku akihusishwa kutimkia Azam Fc jambo ambalo Yanga walimkatalia na kudai kuwa wana mkataba nae mpaka mwaka 2024 hivyo hawezi kuondoka.

SOMA NA HII  MORRISON ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA