Home Habari za michezo KISA TAIFA STARS….TIMU YA LIGI KUU YAMTIMUA KOCHA MKUU…

KISA TAIFA STARS….TIMU YA LIGI KUU YAMTIMUA KOCHA MKUU…

Taifa Stars leo

Klabu ya Geita Gold leo imetangaza kuachana na kocha wake mkuu, Hemed Suleman ‘Morocco’ huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kubanwa na majukumu ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayotarajia kuanza Januari mwakani, nchini Ivory Coast.

Geita Gold imetoa taarifa kwa umma leo Desemba 20, 2023 ikitangaza kuachana na kocha huyo ambaye amedumu klabuni hapo kwa miezi sita tangu alipotambulishwa Julai 21, mwaka huu kuchukua mikoba ya Fredy Felix ‘Minziro’.

Klabu ya soka ya Geita Gold inapenda kuutangazia umma kuwa imefikia maridhiano ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha mkuu wa timu yetu kocha Hemedi Suleiman ‘Morocco’ “Klabu imeridhia ombi la Morocco kusitisha mkataba kwa sababu alizozitaja ikiwa ni pamoja na kubanwa na majukumu ya timu ya Taifa. Klabu inamshukuru kwa kipindi chote alichohudumu kama kocha mkuu wa klabu yetu kwa mafanikio makubwa na pia itaendelea kumtumia kama mshauri wa klabu katika mambo ya kiufundi,”

Morocco ambaye ni kocha msaidizi wa Stars, ameiongoza Geita Gold katika michezo 12 ya Ligi Kuu akishinda mitatu, sare nne na kupoteza tano, akivuna pointi 13 na kukamata nafasi ya 13, huku kikosi chake kikifunga mabao nane na kuruhusu 14.

Pia ameisaidia timu hiyo kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 5-0 mbele ya Singida Cluster.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ALALAMIKA HUKU AKIWAPA ONYO YANGA!!! NOMA KWELI