Home Habari za michezo DILI LA YANGA NA NMB USIPIME….ACHANA NA KADI TU..ISHU YA UWANJA NA...

DILI LA YANGA NA NMB USIPIME….ACHANA NA KADI TU..ISHU YA UWANJA NA MENGINE YAKO HIVI…

Habari za Yanga leo

KLABU ya Yanga SC, imeingia mkataba wa miaka miwili na benki ya NMB kwa ajili ya ushirikiano katika maeneo manne ambayo ni usajili wa Wananchama na mashabiki, miundombinu, biashara na kimfumo.

Licha ya kwamba thamani ya mktaba huo kufichwa, rais wa klabu hiyo, Hersi Said ameeleza namna ambavyo mashabiki na wanachama watanufaika ikiwa ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ambazo zilikuwa zikiwasumbua kwenye mfumo wa usajili wa Kidigitali.

“Katika changamoto kuu mbili ambazo tulikuwa tunapitia za usajili na mwanachama au mashabiki kulipia ada yake na kutopata kadi yake kwa wakati leo napenda kukiri kwa Wanachama na Mashabiki wetu kwamba changamoto hizo tumezipatia suluhisho kwa kuingia ushirikiano na NMB,”

“Yanga itaenda kunufaika katika mradi huu kwa kuhudumia usajili wa Wanachama wao nchi nzima, kupata kadi kwa wakati lakini jambo la tatu kaka yangu (Filbert) atatueleza jinsi gani Wanachama watanufaika na mahusiano haya wakifungua akaunti wakati wakifurahia huduma,” amesema na kuongeza;

“Wanachama wote ambao wameshajisajili kwenye mfumo, huduma ya kwanza ambayo itapatikana NMB ni kuhuisha uanachama wake, takwimu ambazo tupo nazo tumeshashea na wenzetu, huduma ya pili, mtu ambaye sio mwanachama wa Yanga anaweza kwenda tawi lolote la karibu kwa ajili ya kujiunga na uanachama kwa kupata kadi ambayo pia itamsaidia kwa matumizi mengine na itakuwa na muonekano wa uanachama wa Yanga. “

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi (NMB), Filbert Mponzi, amesema; “Kuna huduma mbalimbali ambazo Rais amezisema lakini kubwa zaidi ni kurahisisha huduma kwa Wananchi,”

“Watakuwa wakienda kwenye matawi yetu ni kama wapo nyumbani vile, hii inakuwa sio kadi tu ya kujitambulisha lakini pia unaweza kutumia kwa matumizi mengine ndani ya nje ya nchi huku ukifurahia kuwa shabiki na mwanachama wa timu yako ya Yanga.”

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here