Home Habari za michezo VYUMA VIPYA KUANZA KUSHUKA YANGA WIKI IJAYO….UTARATIBU WOTE HUU HAPA…

VYUMA VIPYA KUANZA KUSHUKA YANGA WIKI IJAYO….UTARATIBU WOTE HUU HAPA…

Habari za Yanga leo

Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kujiandaa kupokea taarifa za usajili wa kushtua ambao utawafanya waendelea, kutamba katika soka la Afrika.

Afisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe amesema kuwa Juma lijalo, Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo watapokea taarifa nzuri za usajili na mambo mengine ya maendeleo ya klabu hiyo ambayo yataendelea kutikisa.

“Baada ya kumtangaza kocha mpya Miguel Gamondi, hatua inayofuata ni kwenda kwenye uzinduzi wa jezi ambazo tutazivaa kwa msimu ujao wa mashindano na baada ya hapo ni kuanza kutambulisha majembe mapya ambayo yataitumikia Young Africans kwa msimu ujao, hivi ninavyoongea ‘thank you’ bado hazijaisha tunatembeza kwanza hizo, halafu tunazindua jezi baada ya hapo sasa kazi ya kuleta wachezaji wapya inaanza,” amesema Kamwe.

Amesema kuwa wachezaji watakaosajiliwa si tu kwamba watakuja kuitumikia na kuipa Young Africans mataji, lakini pia wataiongezea thamani klabu hiyo ambayo ni Mabingwa wa Tanzania Bara na Kombe la ‘ASFC’.

“Wananchi wajiandae kupokea wachezaji wa mpira kwelikweli ambao viongozi wamewaongeza kwa ajili ya ku- saka mafanikio ya msimu ujaó, kwa hiyo wasiwe na wasiwasi, uongozi wao unafanya kazi kwa weledi mkubwa, wakae wakijua wiki ijayo itakuwa ni ya furaha sana kwao tunakwenda kufanya mambo makubwa sana na nawahakikishia wiki itaanza na moto itamalizika na moto,” amesema Kamwe.

Amesema pia juma lijalo watakwenda kuingia mikataba na makampuni mbalimbali yatayoidhamini klabu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano yote.

Klabu hiyo itaanza msimu mpya ikiwa na Kocha mpya baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wake, Nasreddine Nabi ambaye hakuongeza mkataba kufuatia ule wa mwanzo kumalizika.

SOMA NA HII  WAKATI KOMBE LA DUNIA LIKIISHA...TECNO HAWAKUACHI HIVI HIVI...MCHONGO WAO MPYA HUU HAPA...