Home Uncategorized AZAM FC KUKIWASHA LEO DHIDI YA KMC

AZAM FC KUKIWASHA LEO DHIDI YA KMC


 AZAM FC inayonolewa na Arstica Cioaba raia wa Romania, leo Agosti 27 inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex.

Lengo la mchezo huo ni kujiweka sawa kwa ajili ya ligi kuu inayotarajiwa kuanza Septemba 6 na Azam FC wao watafungua pazia na Klabu ya Polisi Tanzania.


KMC jana ilicheza mchezo wa kirafiki na Klabu ya Simba, Uwanja wa Uhuru na ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 hivyo leo utakuwa ni mchezo wake wa pili nao pia wakijiweka fiti kabla ya ligi kuanza.
SOMA NA HII  YANGA:TUNAZITAKA POINTI ZA NAMUNGO, MASHABIKI TUPENI SAPOTI