Home Habari za michezo WAKATI SAWADOGO AKISHUSHIWA NYUNDO YA ‘THANK YOU’ LEO…ISHU YA BANDA UHALISIA UKO...

WAKATI SAWADOGO AKISHUSHIWA NYUNDO YA ‘THANK YOU’ LEO…ISHU YA BANDA UHALISIA UKO HIVI…

Habari za Simba

WAKATI Simba wakimpa ‘Thank You’ kiungo Ismael Sawadogo, winga Peter Banda anadaiwa kugoma kupelekwa kwa mkopo katika timu nyingine akitaka avunjiwe mkataba kama hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo.

Awali ilielezwa Banda alikuwa akitakiwa na Azam FC, lakini dili hilo linadaiwa kufa kimya kimya baada ya kusajiliwa Msenegal, Djibril Sillah na sasa mchezaji huyo aliye mkataba na Simba amegeuka ghafla akisema hataki kutolewa kwa mkopo, ila alipwe chake asepe kama hayupo kwenye mipango ya kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Moja ya kigogo wa Simba (jina tunalo), alisema kuwa Banda anataka abakishwe kikosini au apewe chake asepe jumla nchini badala ya kutolewa kwa mkopo katika klabu nyingine.

“Tuna wachezaji wa kigeni wengi hivyo lazima wapungue ili waingie wengine, Banda ni moja yao ambao kocha hajaridhishwa na ufanisi wake. Tulitaka kumpeleka kwa mkopo, lakini amegoma na kuhitaji kubaki au kuvunjiwa mkataba kitru kitakacholazimisha kumlipa pesa,” alisema kigogo huyo na kuongeza;

“Bado hatujaamua mwisho wake kwani kuna ofa ya moja ya timu inamtaka, hivyo kama wataweza kumnunua itakuwa afadhali kwetu.”

Simba tayari imeshata ‘Thank You’ kwa Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Augustine Okrah, Nelson Okwa, Mohamed Ouattara na Victor Akpan.

SOMA NA HII  SIMBA IJAYO NI UTAMU MWANZO MWISHO.....DILI LA MIQUISSONE 'UPDATE' HII HAPA...