Home Habari za michezo KIPA ALIYECHEZA NA MASTAA WAKUBWA DUNIA AFUNGUKA DILI LAKE LA KUJA SIMBA….

KIPA ALIYECHEZA NA MASTAA WAKUBWA DUNIA AFUNGUKA DILI LAKE LA KUJA SIMBA….

Tetesi za Usajili Simba

KAMA mambo yataenda sawa, Mbrazili Caique Luiz Santos da Purificacao (25), muda wowote kuanzia sasa anaweza kutua aridhi ya Tanzania na kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba, huku mwenyewe akifunguka.

Inafahamika kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ndiye aliyependekeza jina la Caique akiamini ataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha chake kutokana na ubora wake, akiziba nafasi ya Beno Kakolanya aliyepewa ‘Thank You’, na kutimkia Singida Fountain Gate FC, sambamba na pengo la Aishi Manula atakayekaa nje hadi mwezi Novemba kutokana na jeraha la nyonga ambalo alifanyiwa upasuaji mwanzoni mwa mwezi huu nchini Afrika Kusini.

Robertinho wakati anampendekeza Caique aliwasisitiza viongozi wa Simba wamshushe kwani anamjua vyema na anaamini ataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na atatoa ushindani mkubwa kwa waliopo (Manula, Salim Ally na Ahmed Feruz) na hapo ndipo vigogo wa timu hiyo wakaanza harakati za kumpata.

“Lazima tusajili kipa, tunataka kila eneo tuwe na watu zaidi ya wawili wenye ushindani na tayari nimewapa uongozi jina la moja ya makipa ninaowataka (Caique), naamini wanalifanyia kazi,” alisema Robertinho.

Hata hivyo, kipa huyo amezungumza moja kwa moja kutoka Brazil na kuthibitisha kuwepo kwa dili hilo huku akisisitiza kutua nchini kama kila kitu kitaenda poa.

“Ni kweli Simba ilinitafuta, kuna mazungumzo na yapo sehemu nzuri. Kila kitu kikienda vizuri basi nipo tayari kujiunga nao muda wowote kuanzia sasa,” alisema Caique aliyemaliza mkataba na timu yake ya Ypiranga RS inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Brazil.

Aidha pamoja na Yprang Caique, katika nyakati tofauti aliwahi kuzichezea timu nyingine za Brazil ikiwemo EC Victoria iliyomkuza katika Akademi yake na CSA pia aliicheza nchini Marekani kwenye klabu ya Rochester Sambamba na Cyprus kwenye klabu ya Ermis Aradippou.

Caique aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Brazil kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20, (Brazil U-20) kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 akiwa kipa namba moja na kucheza na mastaa wa sasa dunianai wakiwemo, Richarson de Andrade wa Tottenham, Eda Miltao wa Real Madrid, Douglas Luiz wa Aston Villa, Lucas Paqueta wa West Ham na Gablriel Magalhes wa Arsenal.

SOMA NA HII  VIBALI VYA NYOTA MPYA WA SIMBA CHIKWENDE BADO, LOKOSA SAFI