Home Habari za michezo BAADA YA KUSHUHUDIA STARS IKIPOTEANA JUZI MBELE YA ALGERIA….POULSEN ASHINDWA KUJIZUIA…AOMBA MECHI...

BAADA YA KUSHUHUDIA STARS IKIPOTEANA JUZI MBELE YA ALGERIA….POULSEN ASHINDWA KUJIZUIA…AOMBA MECHI NNE…


BAADA ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Algeria, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema wachezaji wake walikuwa na wakati mgumu wa kupambana na nyota bora na imara.

Stars juzi ilifungwa mabao 2-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mechi ya pili ya kufuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika, AFCON, zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2023 nchini Ivory Coast.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Poulsen alisema hawakufikia malengo ya kupata ushindi kwa sababu ya timu pinzani kuwa na wachezaji wenye ubora wa hali ya juu.

Alisema licha ya ubora wa wapinzani wao, lakini anawapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kuonesha mchezo mzuri mbele ya timu bora kama Algeria.

“Wachezaji wanatakiwa kupongezwa kwa sababu ni ngumu kucheza na Algeria na ukatawala mpira na kufanya mashambuliza kadhaa, kwa kiwango kilichooneshwa na wachezaji wangu nina imani timu yetu ina mabadiliko makubwa na tutafanya vizuri huko mbeleni,” alisema.

“Tulikuwa na makosa madogo madogo ambayo yalituadhibu, tumeumia hatujapata matokeo na mchezo huu umetupa somo na Septemba itatupa mwanga wa wapi tutakuwa michuano hii ya kufuzu AFCON,” alisema Poulsen.

Alisema kutokana na wachezaji kupambana na hatimaye kupoteza wanaenda kujiuliza wamepoteza vipi na kujiandaa na michuano ya CHAN ambayo kwa sasa iko mbele yao kwa kuanza na Sudan.

Poulsen alisema michuano ya CHAN dhidi ya Sudan watacheza vizuri, lakini pia watatafuta matokeo mazuri na kuibuka na ushindi ili kusonga mbele zaidi.

“Michuano ya CHAN lakini pia anahitaji mechi nne za kirafiki za kimataifa ili kujiandaa na mchezo dhidi ya Uganda ambao ni mechi ya tatu ya hatua ya makundi ya AFCON,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  KOCHA ALIYEIFUNGA SIMBA GOLI 4-0, AOMBA KIBARUA CHA UKOCHA MKUU MSIMBAZI...AHMED ALLY ATOA VIGEZO...